Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge wa Tanzania akutana na Papa Francis

Neema Papa.jpeg Mbunge wa Tanzania akutana na Papa Francis

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera Neema Lugangira amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Papa Francis, mjini Vatican na kupokea mkono wake wa baraka.

Mbunge Lugangira ni miongoni wa wabunge wanaotafuta fursa mbalimbali katika mataifa mengine na kuleta fursa hizo nchini lengo likiwa ni kusaidia Taifa kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

"Mungu ni mwema sana, nimefika nyumbani kwa Baba Mtakatifu Papa Francis na kupokea Mkono wake wa Baraka. Niseme nini Eeh Bwana, Nitamke maneno gani Kinywani, Nikushukuru Jinsi gani? Nisimulie Vipi Mimi?, Mapito niliyopita maishani?, Nikutukuze Vipi Mungu? Niseme tu Asante Mungu," aliandika Neema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Jana (juzi) ilikuwa siku kubwa sana na ya kihistoria katika maisha yangu. Nimepata fursa ya kushiriki Misa Takatifu katika kanisa la St. Peter's Basilica Vatican ambapo ndilo kanisa alipo Papa Francis," alisema mbunge huyo.

Tayari, Mwadham Kardinali Christoph Schonborn ameshakubali kumsaidia Mhe Lugangira kuanzisha maktaba katika shule za Bukoba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live