Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka utitiri wa makanisa udhibitiwe

Operanews1699371146877 Kilumbe Ng’enda.

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda (CCM) ameiomba  Serikali iweke mkazo katika usajili wa makanisa na taasisi za dini za madhehebu mbalimbali, ili kudhibiti yanayodaiwa kufundisha imani zenye madhara kwa jamii.

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 7 Novemba 2023, Ng’enda alidai kumekuwa na utitiri wa makanisa na taasisi nyingi za dini, kutokana na kukosekana kwa udhibiti katika usajiri wake.

“Serikali inapaswa kuweka usajili katika taasisi na madhehebu ya dini, hiyo itasaidia kupunguza madhara yanayoletwa na taasisi hizo,” amesema Ngenda.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini amesema usajili wa taasisi hizo unafanywa kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya na kwamba kabla hazijasajiliwa hupitiwa ili kubaini kama zimekidhi vigezo.

“Ofisi ya Msajili inaendelea kushughulikia maombi ya usajili wa taasisi na madhehebu ya dini na kutoa usajili kwa wakati kwa taasisi zenye sifa stahiki. Lakini kuhakikisha Serikali haisajili taasisi  ambazo zinaweza kuleta madhara kwa jamii na kuhamasisha vitendo ambavyo ni kinyume na mila na maadili ya kitanzania,” amesema Sagini.

Sagini, amesema jumla ya maombi ya usajili wa taasisi na madhehebu ya dini 1,858 yalipokelewa katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya, ambapo taasisi 419 zilisajiliwa, wakati maombi ya taasisi nne yakikataliwa huku maombi 1,435 yakiwa katika hatua mbalimbali za usajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live