Dar es Salaam. Mbunge wa Segerea (CCM), Bonnah Kamoli ameomba kuundwa kamati kuchunguza ujenzi wa kituo cha polisi Segerea kilichoanza kujengwa mwaka 2017.
Kamoli ametoa kauli hiyo jana Jumatatu Julai 22, 2019 katika ziara yake katika kata za jimbo hilo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za mfuko wa jimbo, Serikali na wafadhili.
Amesema katika ujenzi huo alitoa mabati 60, naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akitoa Sh500,000 na mkuu wa majeshi nchini (CDF), Venance Mabeyo alichangia Sh3 milioni.
"Kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa kituo hiki cha polisi Segerea hii ni ishara za ubadhirifu, kupitia mkutano wa halmashauri kuu ya CCM kata ya Segerea natoa maelekezo ya kuundwa kwa kamati kuhusu ujenzi huu ili kubaini ukweli wake,” amesema Kamoli.
Katika hatua nyingine, Kamoli amewasisitiza mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya maji katika kata ya Segerea.
Amewataka kuzingatia ubora wa kazi wanayoifanya ili kufikia Oktoba, 2019 wakazi wa kata ya Kipawa waanze kupata huduma ya maji safi na salama.
Pia Soma
- Majaliwa kufungua mkutano Alat
- Polisi wachunguza sauti zinazodaiwa za makada wa CCM
- Uingereza kuijadili Iran kwa dharura