Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Haonga aachiwa kwa dhamana

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Mbozi ( Chadema), Pascal Haonga ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi tangu jana usiku baada ya kukamatwa nje ya geti la kuingilia viwanja vya Bunge.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Mei 7, Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini amesema Haonga ametakiwa kuripoti polisi Alhamisi.

Asubuhi Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika aliomba kutoa hoja bungeni chini ya kanuni 47 ili Bunge lijadili kukamatwa kwa mbunge huyo.

Mnyika amesema Spika wa Bunge, Job Ndugai alitoa mwongozo kuwa polisi kukamata wabunge wakati kipindi cha Bunge kikiendelea ni  kinyume cha haki za Bunge.

“Lakini jana usiku wakati akitoka bungeni getini polisi walimkamata Mbunge wa Mbozi mheshimiwa Haonga na limemlaza ndani hadi leo,” alisema.

Mnyika alisema wakati kipindi cha maswali kikiendelea, alikwenda na Haonga hadi nje ya geti la Bunge kwa ajili ya kuwaomba wabunge wengine kuondoka naye kwenda nyumbani kwake kwa ajili ya ukaguzi.

Habari zinazohusiana na hii

“Wanaenda kum search (kumkagua) kwa kile kinachodaiwa kuandika ujumbe tu Mei mwaka 2018 kwenye kundi la mtandao wa wabunge la Whatsapp,” alisema.

Mnyika alisema  vitendo vya polisi kukamata wabunge wakati vikao vya Bunge vikiendelea vimekithiri hivyo anaomba atoe  hoja jambo hilo lijadiliwe na Bunge.

“Na mheshimiwa Haonga aachiwe mara moja aendelee na kazi zake za Bunge na utaratibu ufuatwe kama vile Spika alivyotoa mwongozo,”amesema.

Akijibu, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alisema hoja hiyo haiwezi kukubaliwa kwasababu Spika Ndugai hana mamlaka hayo.

“Mwongozo wa Spika ni kwamba mtu yeyote ambaye anatakiwa kukamatwa ndani ya Bunge ndiyo kibali kitoke lakini nje ya Bunge Spika hana mamlaka hayo,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz