Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Bwege alilia masheikh wa Pakistani kutimulia nchini

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungala ‘Bwege’ amelalamikia masheikh saba kutoka Pakistan kuzuiliwa na Idara ya Uhamiaji kutoa huduma za kidini katika jimbo lake mkoani Lindi.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili Septemba 30, 218 jijini Dar es Salaam Bwege amesema maofisa wa uhamiaji waliwakamata masheikh hao Septemba 14, 2018 kwa madai hawana kibali kutoka kwa Mufti na walitakiwa kuondoka nchini Septemba 27, 2018 hawakuondoka na leo wamepewa siku ya mwisho kuwapo nchini.

Amesema alifanya jitihada za kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na kumweleza suala hilo lakini naye akasisitiza masheikh hao hawakuwa na kibali kutoka kwa Mufti.

"Masheikh hao walikuwa na vibali vyote na walitambuliwa na (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania) Bakwata na barua walikuwa nayo. Ninajiuliza nani mwenye mamlaka ya kutambua uhalali wa wageni wanaoingia nchini, Mufti au Uhamiaji?" Amehoji mbunge huyo.

Amesema watu wake wananyimwa uhuru wa kupata mawaidha kutoka kwa viongozi wa kidini, jambo ambalo ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi. Amesema masheikh hao walikuwa wakifundisha dini na siyo kitu kingine.

Bwege amesema hakuna sehemu ambayo wameongelea masuala ya kisiasa katika mafundisho yao.

"Namuomba Rais John Magufuli aangalie mwenendo wa Serikali yake katika mambo ya kidini kwa maslahi mapana ya Taifa," amesema Bungala.

Mbunge huyo amewataja masheikh hao kuwa ni Gulman Ullah, Maikman Ullah, Hikmat Ullah, Atta Ullah, Nek Mohammad Khan, Badshah Khan na Arbab.

Chanzo: mwananchi.co.tz