Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumaini ya wahamiaji Morocco mikononi mwa Papa

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wahamiaji kwenye kambi iliyopo jijini Casablanca wana matumaini madogo kuhusu hali yao ya baadaye, baada ya ndoto zao za kupata maisha mapya barani Ulaya kukatishwa huku wakisubiri kuona kama ziara ya Papa itawaokoa.

Kambi isiyo halali lakini inayovumiliwa ya Oulad Ziane ni ya mwisho ya aina yake nchini Morocco baada ya kuvunjwa kwa kambi kama hiyo katika mji wa Kusini wa Agadir mwezi Machi na nyingine iliyo katikati ya mji ya Fes.

"Haya si maisha. Tulichonacho ni Mungu tu," alisema Marcelin, mhamiaji kutoka Cameroon ambaye amekuwepo nchini Morocco kwa miaka mitano na sasa amekwama kwenye kambi hiyo baada ya majaribio yake kadhaa kwenda Ulaya kushindikana.

"Hatutegemei chochote kutoka kwa yeyote, lakini matumaini yetu usalama kidogo na usafi kwa watoto," alisema raia huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 30.

Alikuwa akizungumza kabla ya ziara ya Papa Francis nchini Morocco inayoanza Jumamosi, huku kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani akiwa ameweka suala la uhamiaji kama moja ya ajenda zake kuu katika ziara hiyo ya kihistoria.

Katika ujumbe uliotumwa jana Alhamisi, Papa alisema atakutana na "wahamiaji ... ambao wanawakilisha haja ya kujenga pamoja dunia yenye haki na usawa".

Kambi ya Oulad Ziane, ambayo ina wahamiaji kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni sehemu ambayo imegubikwa na simanzi na kukata tamaa.

Idadi ya wahamiaji kwenye kambi hutofautiana lakini huzidi watu 2000, alisema Lassine Camara, ambaye anajiita "rais" wa jumuiya ya raia wa Mali na msemaji wa wananchi kutoka Cameroon, Guinea, Ivory Coast, Nigeria, Senegal na nchi nyingine.

Wahamiaji hao hujisitiri katika nyumba za mbao ambazo hufunikwa na mablanketi au vipande vya plastiki.



Chanzo: mwananchi.co.tz