Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maskofu zaidi ya 10 kuendesha misa mazishi ya Magufuli

Za 0 Maskofu zaidi ya 10 kuendesha misa mazishi ya Magufuli

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Chato mkoani Geita Leo Machi 25,2021, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu,  Jenister Mhagama amesema misa hiyo itaanza asubuhi katika uwanja huo.

Amesema kabla ya mwili wa hayati Magufuli kupelekwa uwanjani hapo, utasaliwa katika Kanisa alilobatizwa mjini Chato la Parokia ya Bikira Maria.

Mhagama amesema maziko ya hayati Magufuli yataongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan nyumbani kwa marehemu.

Ameongeza kuwa baada ya shughuli za maombi kukamilika shughuli za maziko zitafanyika leo jioni wilayani Chato mkoani Geita

Aidha, amewapongeza waandishi wa habari kwa kazi waliyofanya katika kipindi chote tangu kifo hicho kilipotangazwa.

Amesema waandishi wa habari walilipoti habari hizo bila kuchoka usiku na mchana.

Chanzo: ippmedia.com