Mamia wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wamejitokeza katika uwanja wa Taifa kushuhudia mashindano makubwa ya usomaji Qur’an.
Mashindano hayo ya 23 yanajumuisha jumla ya washiriki 23 kutoka nchi 23 ndani na nje ya bara la Afrika.
Miongoni mwa nchi hizo ni za Afrika Mashariki pamoja na za Afrika Magharibi kama vile Nigeria.
Pia, kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, kuna washiriki kutoka bara la Asia kama Saudi Arabia lakini vile vile Marekani na Uingereza.
Atakaeibuka kidedea katika mashindano haya atajizolea zawadi ya kitita cha fedha taslimu milioni 23 za kitanzania ambazo ni sawa na dola elfu 10 za kimarekani.
Mshindi wa pili hadi wa tano watapata kuanzia milioni 15 hadi milioni 4.
Licha ya mvua kubwa inayonyesha idadi kubwa wa wananchi walionyesha utulivu mkubwa kufuatilia mashindano hayo huku wakinyeshewa.
Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ndio anamwakilisha mgeni rasmi ambae ni rais Samia Suluhu Hassan.