Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapadri wataka viongozi kuombewa, wakemea ushoga

33363 Pic+padre Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Paroko wa Kanisa Katoliki la Epiphania Bugando jijini Mwanza, Padri Valentine Kavalo amesema kuna haja ya kuwaombea viongozi wa Serikali wasiothamini dini ili kuwa na moyo wa huruma na kusamehe.

"Tuombee amani maana kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani ili usiwe na vurugu,”  amesema Padri Kavalo jana usiku Desemba 24, 2018 katika misa ya mkesha wa Krismasi.

Wakati Kavalo akieleza hayo, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Renatus Mkwande amesema Watanzania wanapaswa kupiga vita vitendo viovu vikiwemo vya ushoga, wanafunzi kutoa mimba na rushwa badala ya kuwaachia viongozi wachache washughulike nayo. 

"Wanaume wanajigeuza wanawake na wanawake wanajigeuza wanaume, tukatae.  Wakristo wote tuwaunge mkono viongozi wetu kuwapinga mashoga, tusikubali kupokea maovu hayo kwa kigezo cha kupata misaada tukiacha vikaendelea siku moja tutakuja kushangaa mambo yakibadilika," amesema.

Amesema wapo wazazi wanaoshiriki kutenda dhambi kwa kushiriki watoto wao kutoa mimba.

"Watoto wetu wanaachwa bila malezi, wazazi hawana muda nao wanajilea wenyewe, baba anarudi usiku nyumbani amelewa mtoto naye utakuta saa mbili yupo tu mitaani anafanya ayajuayo yeye. Lazima tuwalee watoto wetu katika uadilifu na tuliombee Taifa letu. Utandawazi hautaacha dunia salama,” amesema.

Amesema yapo mashirika mengi yanayotetea haki za watoto lakini hakuna shirika linalotetea watoto ambao bado hawajazaliwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliomba ushirikiano baina ya taasisi za dini na Serikali bila kujali itikadi zao huku akiwahakikishia usalama wakati wa kusherehekea sikukuu hizo.



Chanzo: mwananchi.co.tz