Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno machafu yapigwa marufuku, mwezi wa mfungo

Shekhees Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Sheikh Husein Maneno Simo

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Sheikh Husein Maneno Simo ametoa wito kwa Waislam wote nchini kuendelea kulinda amani iliyopo na kuwa wazalendo.

Sheikh Huseni ameyasema hayo hivi karibuni, katika Msikiti wa Azhar uliyopo Kata ya Kivinje Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi ambapo amewataka Waislamu wote kujivunia amani iliyopo nchini na kuwataka watende matendo mema ambayo yanamfurahisha Mwenyezi Mungu.

“Katika Mwezi wa Ramadhani Waislam wote wanatakiwa kutosema maneno machafu, kutokufanya matendo maovu ambayo yanahatarisha amani ya nchi na matendo mengine ambayo uislamu haukubaliani nayo ’’alisema Sheikh Huseini.

Alisisitiza kuwa uislamu ni dini ambayo kwa sehemu kubwa inahimiza amani kama ilivyo jina lake al islam lenye maana ya amani.

“Hivyo sisi kama Watanzania kama wanakilwa na kama waislamu ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba amani ya Tanzania inakuwa kipaumbele na amani ya Kilwa inakuwa kipaumbele’’ alieleza Sheikh Huseini.

Pamoja na hayo, ameongeza Serikali hivi saaa inatengeneza miundombinu kwaajili ya kuwasaidia wananchi lakini uharibifu unafanywa na mingoni mwetu hivyo ni wajibu wa kila muislamu kutumia mwezi wa ramadhani kutenda matendo mema na kuwa mzalendo wa taifa hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live