Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wakusanyika kumuaga Askofu Ruwaich

15209 Pic+askofu TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza wameungana pamoja katika makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo Kawe kamo Jijini Mwanza kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa askofu wa Jimbo jilo Jude Thaddeus Ruwaich.

Askofu Ruwaich aliteuliwa na Papa Francis kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam Juni 22, 2018.

Akiongoza misa ya kumuaga askofu huyo leo Septemba 2, 2018, Askofu Mkuu Jimbo la Tabora, Paul Ruzoka amesema askofu Ruwaich ameliongoza jimbo hilo kwa miaka minane.

Askofu Ruzoka amesema Askofu Ruwaich atasimikwa rasmi na kuanza kutumikia huduma hiyo Septemba 7, 2018.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Ruwaich amewaasa waumini wa kanisa hilo pamoja na askofu atakayeteuliwa kumrithi kulisoma neno la Mungu mara kwa mara.

“Jambo hili nimekuwa nikiwakumbusha mara kwa mara ndani ya utume wangu kwa miaka nane tangu nilipoteuliwa kuwa askofu wa jimbo hili, lakini pia mfuate sheria za kanisa na kuepuka sheria za mtu anayeibuka nazo kusikojulikana,” alisema Askofu Ruwaich.

Askofu Ruwaich amewaomba waumini hao kuombea kazi yake anayoenda kuifanya na kwamba ataendelea kuwaombea waumini wa kanisa hilo jimbo la Mwanza.

Misa hiyo imehudhuriwa na askofu wa Jimbo kuu la Tabora, mapadre wa parokia zote na waumini toka parokia mbalimbali na majimbo tofauti ya Mwanza.

Mbali na misa hiyo, pia askofu huyo atashiriki kukabidhi vyeti kwa shule 10 za vijana wa TYCC zilizofanya vizuri.

Chanzo: mwananchi.co.tz