Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda anavyomwaga machozi madhabahuni

25632 Makonda+pic TanzaniaWeb

Tue, 6 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kwa wanaomfuatilia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda si kitu cha ajabu kuona machozi yake hasa linapotokea jambo linalomtikisa.

Wakati wa sakata la dawa za kulevya, Makonda alimwaga machozi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kimara jijini Dar es Salaam alipokwenda kusali akiomba aombewe kutokana na kuwagusa wanaohusika na dawa hizo.

Akiwa mbele kwenye madhabahu, Makonda alipewa nafasi ya kuzungumza ndipo alipozungumzia suala hilo na kujikuta akilia kwa uchungu.

Agosti 26, 2018 akiwa Kanisa la Anglikana mjini Ngara, Makonda alitoa onyo kwa atakayenunua makontena yake kuwa atapata laana yeye na uzao wake.

Alisema atasali na kuomba kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa kuwa anaamini Mungu alimpatia kwa ajili ya walimu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Hiyo ni baada ya uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupiga mnada makontena yake yaliyokuwa na vifaa vya thamani za shule alizoagiza kwa ajili ya walimu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kama hiyo haitoshi, jana Jumapili Novemba 4, 2018 wakati wa kampeni yake ya kupambana na mapenzi ya jinsia moja (ushoga) ikipingwa ikiwamo Serikali, alikwenda  Kanisa la Efatha jijini Dar es Salaam na kurudia kitendo hicho cha kumwaga machozi.

Alianza kwa kusema; Mungu hana furaha na yeye kwa kuwa kuna ongezeko la idadi ya madanguro na mashoga katika mkoa wake.

“Nimekuja mbele zenu kwa ajili ya kutubu, naomba toba kwa ajili ya mkoa wangu, nahitaji Mungu auponye mkoa wangu, nahitaji awaponye watoto wa mkoa huu, watoto wanaumia sheria ipo, lakini haizingatiwi.”

“Neno la Mungu halienei kama yanavyoenea madanguro na bar, watu wanaomba uongezwe muda wa kufanya uzinzi na sio kuhitaji muda wa kumuomba Mungu, nimekuja kwako baba kuomba uniombee na uuombee mkoa wangu nahitaji rehema katika mkoa,” alisema Makonda huku akilia.

Soma zaidi: Serikali ya Tanzania yamkana Makonda

Chanzo: mwananchi.co.tz