Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda amtembelea Mufti wa Tanzania

Makondaaa 3965 Makonda amtembelea Mufti wa Tanzania

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda, leo tarehe Mosi Desemba 2023, amemtembelea Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakary Zuberi bin Ally ambaye amemfanyia dua maalum.

Makonda alifika kumshukuru Mufti kwa kumuombea na kuwa pamoja naye katika nyakati zote alizozipitia na kuomba baraka zaidi katika maisha na shughuli zake.

Kiongozi huyo wa CCM amefanya hivyo kama muendelezo wa ushirikiano wa karibu na kikazi na viongozi wa dini, kwa kutambua nafasi yao katika kuliombea taifa amani na ustawi.

Mufti Dkt. Abubakary Zuberi bin Ally amemuahidi Makonda kuendeleza ushirikiano na kuombea kuhakikisha anafanya kazi zake vyema kwa lengo la kumsaidia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live