Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi yavamia kanisani, yapora sadaka

5825 ST.THERESIA TZW

Thu, 5 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

Majambazi wamevamia Parokia ya Mtakatifu Theresia, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo na kupora sadaka na vikombe vitano vya misa, usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa Padre wa Dekania ya Kibaha ya Kanisa Katoliki, Fr Benno Kikudo, walinzi wa Parokia walipigwa na kuumizwa ila hawakuweza kuifikia nyumba ya mapadre. “Usiku wa kuamkia leo, mapadre wenzetu wa parokia ya Mt Theresia, Mbezi Mwisho waliingiliwa na majambazi kanisani.

Majambazi walivunja mlango wa sakristia. Wameiba sadaka na vikombe vitano vya misa. Majambazi waliwapiga na kuwaumiza walinzi wa parokia. Bahati nzuri hawakuingia nyumba ya mapadre,” ameandika Fr Kikudo. “Baba Paroko Fr Sunnil amenipatia taarifa asubuhi hii. Tumpatie pole Baba Paroko na mapadre wote pole,” ameongeza katika taarifa yake

Chanzo: habarileo.co.tz