Dar es Salaam. Waziri Mkuu, kassim Majaliwa amesema utulivu na uadilifu ulioonyeshwa na Waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhan unatakiwa kuendelea kila siku.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 5, 2019 katika maadhimisho ya baraza la Eid El Fitri lililofanyika Mkoa wa Tanga.
Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amesema katika mwezi huo Waislamu wamekuwa si tu raia bora, bali wanapaswa kutolewa mfano.
“Katika kipindi cha swaumu mmeonyesha upendo, usafi na nia ya moyo hata baada ya kumalizika kipindi cha ramadhani natamani muendelee hivyo, niwaambie kuwa hatutakoma kuendeleza yale mazuri tuliyotenda mwezi huu, mshikamano huu na maisha yanayotufanya tuwe wamoja.”
“Ni matarajio yangu katika miezi 11 ijayo kabla ya ramadhani nyingine tutaendelea kuishi kwa amani, upendo na mshikamano kama ilivyokuwa sasa," amesema Majaliwa.
Amesema utulivu na uadilifu ulioonyeshwa ni silaha muhimu ya kupambana na maovu na uhalifu katika jamii.
Pia Soma
- 41 warejesha fomu kuwania udiwani, 29 wapita bila kupingwa
- Sugu ataja sababu nne za kutong’oka ubunge Mbeya
- VIDEO: Mama wa watoto wanne amsamehe mumewe aliyempa talaka