Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa aongoza mazishi ya Sheikh Yahya

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana Jumanne, Machi 5, 2019 amewaongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika mazishi ya Imamu wa Msikiti wa Mtoro, Sheikh Zubeir Yahya Mussa yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu.

Sheikh Zubeir ambaye ni miongoni mwa masheikh maarufu jijini Dar es salaam alifahamika sana kutokana na kuwa imamu wa msikiti huo ambao ni miongoni mwa misikiti mikubwa na maarufu zaidi hapa nchini, alifariki dunia juzi usiku.

Pamoja na uimamu wake, Sheikh Zubeir aliwavutia watu wengi sana kutokana na mahubiri yake aliyokuwa akiyaendesha kwa ufundi mkubwa katika msikiti huo na maeneo mengine.

Sheikh Zubeir alikuwa miongoni mwa masheikh waliojiweka karibu na jamii na kuwa na uhusiano mzuri na masheikh wenzake kutoka taasisi mbalimbali.

Sheikh Zubeir alipata elimu yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Madina, (Ummul- Quraa) akiwa pamoja na Sheikh Juma Omar Poli, Sheikh Muharram Juma Doga, Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir na wengineo.

 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega; Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Jumaa; Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.



Chanzo: mwananchi.co.tz