Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa aagiza waliohujumu mradi wa kijiji wakamatwe

12341 Pic+majaliwa TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Ally Mkalipa kuwakamata waliohusika katika ubadhirifu uliofanyika kwenye mradi wa mashine ya kukobolea mpunga ya kijiji cha Chomachankola wilayani humo.

Ametoa kauli hiyo jana jioni Alhamisi, Agosti 16, 2018 baada ya mbunge wa Manonga, Seif Gulamali kulalamikia kuhusu fedha zilizotolewa kwa ajili ya mradi wa mashine ya kukoboa mpunga ya kijiji hicho, ambazo zilitolewa miaka mitano iliyopita lakini hadi sasa mradi haujaanza.

Imeelezwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Igunga ilitoa Sh35milioni ili kukiwezesha kijiji hicho kununua mashine ya kukoboa mpunga lengo likiwa ni kuwawezesha wakulima kuliongezea thamani zao hilo kwa kukoboa mpunga na kuuza mchele.

Majaliwa ameagiza katibu wa kamati ya mradi huo,  Daudi Mwangaluka, John Fumbuka (mjumbe), Yusta Thomas (mweka hazina) na Hansa (mkandarasi) kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Amesema Serikali haiwezi kukubali kuona fedha za wananchi zilizotolea kwa ajili ya miradi ya maendeleo zikitafunwa na watu wachache wasiokuwa waaminifu, ambao wanakwamisha ukuaji uchumi wa kijiji.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekemea vitendo vya watoto wa kike kukatishwa masomo kwa kupewa ujauzito na amewata wazazi na walezi wilayani hapa wahakikishe wanasimamia elimu ya mtoto wa kike ili aweze kumaliza masomo yake.

Waziri Mkuu alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila usumbufu wowote na atakayebainika kukatisha masomo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz