Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahujaji waruhusiwa kuingia Mecca kwa mara ya kwanza

9a0dd4795fe4d84aed99729cecb92e3e Mahujaji waruhusiwa kuingia Mecca kwa mara ya kwanza

Mon, 2 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAHUJAJI wa nchi za nje jana wameruhusiwa kufika kwenye msikiti mkuu mjini Mecca kwa mara ya kwanza tangu kuanza kutekelezwa kwa masharti ya kukabiliana na Corona miezi saba iliyopita.

Kuanzia jana Jumapili, baadhi ya mahujaji 10,000 kutoka nje ya nchi wameruhusiwa kufanya ibada ya Hija ya Umrah ambayo waislamu huweza kuitekeleza kipindi chochote kile.

Mahujaji hao walilazimika kujitenga kwa siku tatu baada ya kuwasili Saudi Arabia kabla ya kuruhusiwa kuzunguka Kaaba – eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiislamu – katikati ya msikiti mkubwa.

Saudi Arabia imeripoti maambukizi 347,282 ya ugonjwa wa Covid-19 huku ikirekodi vifo 5,402 tangu kuanza kwa janga la virusi vya corona ilihali watu 333,842 wakithibitishwa kupona.

Nchi hiyo imeanza kufungua baadhi ya misikiti kama sehemu ya kulegeza masharti kote nchini humo.

Chanzo: habarileo.co.tz