Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maharusi 70 wa Sheikh Kishk walivyotinga ukumbini

Kishki Picg Maharusi 70 wa Sheikh Kishk walivyotinga ukumbini

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ni miongoni mwa wageni waliowasili kushuhudia hafla ya ibada ya kufungisha ndoa 70 za vijana waliofadhiliwa na taasisi ya Al-Hikma kutimiza ibada hiyo katika Dini ya Kiislamu.

Tukio hilo ambalo ni aghalabu kutokea nchini linafanyika leo Jumapili Agosti 06, 2023 katika Ukumbi wa DYCCC Hall Temeke jijini Dar es Salaam likifadhiliwa na taasisi hiyo inayoongozwa na Sheikh Nurdin Kishk.

Jumla ya mabwana harusi 70, wakiwa wamevalia majoho meusi na kanzu nyeupe  waliowasili ukumbini hapa saa 9. 37 asubuhi wakishuka kwenye mabasi aina ya  Coster tatu zilizowabeba kisha walijipanga mistari miwili na kuingia ukumbini hapa wakiwa na sura za furaha.

Ndoa katika Uislamu ni mapatano ya kisheria za kidini kati ya jinsia mbili mwanaume na Mwanamke na inafungwa Kwa taratibu za kidini ambapo Kuna kuwa na cheti cha kimaandishi mbele ya mashahidi wawili na mlezi wa bibi harusi na bwana harusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live