Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli ataka shughuli za kidini kutofungwa mkoani Kilimanjaro

Video Archive
Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,  Anna Mghwira amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtaka kutofunga shughuli za kidini mkoani humo bali ashughulikie upungufu uliojitokeza katika kongamano la Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa lililosababisha vifo vya watu 20 na 16 kujeruhiwa.

Mghwira ameeleza hayo leo Jumatatu Januari 3, 2020 wakati wa kuaga miili ya watu 18 waliokufa katika kongamano hilo lililofanyika Jumamosi Februari Mosi, 2020 mjini Moshi.

Mwamposa anadaiwa kuendesha ibada na kuwaelekeza waumini wake kukanyaga mafuta yaliyokuwa yamemwagwa juu ya kasha ambalo ndani  yake lilitandikwa plastiki zito lililomwagiwa mafuta, jambo ambalo inadaiwa lilichangia vifo hivyo na majeruhi.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema baada ya kuwasiliana na Rais Magufuli leo asubuhi alimueleza kushughulikia upungufu uliojitokeza na asifunge shughuli za dini.

“Huu ndio ujumbe wa Rais ambao naona sisi sote tuliokuwapo hapa tunakubaliana nao, yakwamba tuendelee kumtafuta Mungu lakini mapungufu yetu ya kibinadamu tuyashughulikie, kwamba tushughulikie mapungufu na tusifunge shughuli za imani,” amesema.

Amewataka viongozi wa dini na wasio wa dini kuzingatia taratibu katika kufanya mihadhara ikiwemo kuzingatia muda.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Nawaomba viongozi wa dini kuwa chachu ya maarifa ya amani, upendo wa kweli na hali ya kujali watu pia mihadhara yote ya dini na isiyo ya kidini zifuatwe taratibu kwa kiwango cha hali ya juu, muda wa kuanza na muda wa kumaliza lazima uzingatiwe,” amesema Mghwira

Chanzo: mwananchi.co.tz