Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli aelezwa madhara ya michezo ya kubahatisha

38022 PIC+KUBETI Magufuli aelezwa madhara ya michezo ya kubahatisha

Wed, 23 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora Tanzania, Zainuddin Adamjee ameshangazwa na tabia ya vyombo vya habari kufanya matangazo ya michezo ya kubahatisha licha ya kuwa ni haramu katika dini zote.

Adamjee akizungumza leo katika kikao kati ya Rais John Magufuli na viongozi wa madhehebu ya dini Ikulu jijini Dar es Salaam amesema hivi sasa vijana wengi nchini ambao ni nguvu kazi ya Taifa wanacheza kamari kila dakika kwa sababu kila ukifungua televisheni ni matangazo ya michezo hiyo.

“Mambo mengi yanazungumzwa hivi sasa ni kamari tu, kauli yako ya ‘Hapa Kazi tu’ kwa hizi kampuni ni hapa kamari tu. Utaona vijana wengi badala ya kufanya kazi wanacheza kamari.”

“Mtu anatumia zaidi ya Sh10,000 kucheza kamari halafuhuyo anayeshinda utaona anapewa zawadi na mkuu wa mkoa au wilaya na anapoambiwa (aliyeshinda) sema chochote anasema mimi sikuamini sasa naamini watu waendelee kucheza,” amesema.

Amesema wakati Taifa likiangalia matatizo yako wapi asitafutwe mchawi kwa sababu shida ni kuwa nguvu kazi inacheza kamari.



Chanzo: mwananchi.co.tz