Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli Kanisani "Watanzania tulime ili tuwasaidie wanaosumbuliwa na corona"(+picha)

102526 Pic+magu Magufuli Kanisani

Sun, 17 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Januari, 2021 ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria, Parokia ya Chato Mkoani Geita kusali Misa Takatifu (Dominika ya 2 ya Mwaka B) iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Henry Mulinganisa.

Akitoa salamu katika Misa hiyo, Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amewapongeza Waumini wa Kanisa hilo kwa kufanikisha upanuzi wa Kanisa lao ambalo sasa lina nafasi ya kutosha Waumini wengi zaidi kufanya Ibada kwa wakati mmoja.

Rais Magufuli ametoa wito kwa Waumini hao na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake kwa Taifa na hasa kwa kuepusha janga la ugonjwa wa Corona (Covid -19) nchini Tanzania ilihali ugonjwa huo ukiendelea kusababisha vifo vya maelefu ya watu katika nchi nyingine duniani.

Amesisitiza kuwa kutokana na Tanzania kuepushwa na ugonjwa huo, Watanzania wanapaswa kutumia nafasi hii kuchapa kazi zaidi hasa kuzalisha mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya chakula kwa ajili ya kuzisaidia nchi ambazo zinashindwa kufanya uzalishaji kutokana na watu wake kufungiwa majumbani (lockdown) na pia kukuza uchumi.

“Sasa hivi mvua zinanyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, nawaombeni sana ndugu zangu Watanzania tulime mazao hasa ya chakula, tulime kwa wingi ili baadaye tuje kuwasaidia wenzetu ambao wanashindwa kulima kutokana na Corona”  Rais Magufuli.

MAMA WA MWANAFUNZI WA KWANZA KIDATO CHA NNE AFICHUA SIRI “TOKA AKIWA MDOGO NI MDADISI, HAFANYI TU”

Chanzo: millardayo.com