Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yaziacha kaya 59 bila makazi, 100 waomba chakula Mwanza

85801 Pic+mafuriko Mafuriko yaziacha kaya 59 bila makazi, 100 waomba chakula Mwanza

Mon, 25 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sengerema. Kaya 59 wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania zimekosa makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kutokana mvua kubwa iliyonyesha Jumamosi ya Novemba 23, 2019.

Pamoja na kuzingirwa maji kwa makazi hayo, mvua hiyo ilisababisha vifo vya watu kumi na kujeruhi watu watano.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Novemba 25, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema tathimini iliyofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imebaini kaya 59 zimekosa makazi na watu 100 hawana chakula na mahitaji mengine baada ya vitu vyao kusombwa na maji.

Amewaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kujitolea kuwahifadhi watu hao na kutoa michango ya chakula, dawa na vitu vingine kuwasaidia waathirika hao.

Kipole amesema tayari kamati ya ulinzi na usalama imeweka utaratibu wa kupokea misaada ambapo ofisa ya mkurugenzi  wa Halmashauri ya Sengerema pamoja ofisi ya katibu tawala wataratibu shughuli hiyo ya kupokea michango hiyo.

"Tunawaomba watu na taasisi mbalimbali kujitokeza kutoa misaada lengo ni kuwasaidia watu hawa waliokumbwa na mafuriko tuweze kuwasaidia," amesema Kipole.

Mmoja wa watu walionusurika kwenye mafuriko hayo, Raulensia Ibalaja amesema yeye hakuokoa kitu chochote hivyo naiomba Serikali imusaidie  walau chakula ili aweze kuendesha maisha yake.

Mbunge wa Sengerema (CCM) Wiliamu Ngeleja leo atakuwa jimboni kwake kwa ziara ya siku moja ya kuwatembelea watu waliokumbwa na mafuriko kisha kutoa mkono wa pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu zao.

Chanzo: mwananchi.co.tz