Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabaki ya kipekee ya Biblia yapatikana pangoni

8d2af820c282041d991ca060a0a2e9db.png Mabaki ya kipekee ya Biblia yapatikana pangoni

Thu, 18 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MABAKI ya machapisho ya Biblia ya kale yamepatikana katika kile ambacho maofisa wametaja kuwa uvumbuzi wa kihistoria katika mapango ya jangwani nchini Israel.

Makumi ya vipande vya karatasi zilizoandikwa kwa Kigiriki, jina la Mungu likionekana kwa Kihibru yalipatikana katika mapango hayo.

Machapisho hayo yanayoaminiwa kuwa ya waasi wa Kiyahudi waliokimbilia milimani baada ya kuibuka kwa upinzani dhidi ya utawa wa Kirumi katika karne ya pili.

Karatasi hizo zilipatikana wakati wa operesheni ya kuhifadhi eneo hilo la pangoni lisivamiwe.

Katika karatasi hizo maneno yaliandikwa kwa Kigiriki isipokuwa jina la Mungu ambalo liliandikwa kwa Kihibru.

Uvumbuzi huo ni wa kwanza kupatikana tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960 wakati mabaki kama hayo na mifupa 40 ilipatikana katika eneo hilo ambalo limepewa jina la pango la ajabu.

Mabaki yaliyopatikana yana machapisho kutoka ya Zakayo na Nahum ambayo yanajumuisha sehemu ya maandiko yanayojulikana kama kitabu cha mitume 12 wadogo.

Mabaki ya ngozi yalikuwa yameandikwa kwa Kigiriki, lugha iliyotumiwa baada ya ushindi wa Yudea na Alexander the Great katika karne ya nne kabla ya ujio wa Kristo. Jina la Mungu, hata hivyo linaonekana kuandikwa kwa Kihibru.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mambo ya Kale ya Israel (IAA), Israel Hasson alisema mabaki hayo na vitu vingine vilivyopatikana hapo ni ya thamani kubwa kwa binadamu.

Shehena ya shilingi za kale kutoka zama za uasi wa Kiyahudi, Mfupa wa mtoto uliodumu miaka 6,000-na kapu la kale lililotengezwa karibu miaka 10,500 iliyopita pia ilipatikana katika eneo hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz