Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maalim Seif ataka Ramadhan itumike kama chuo cha wema

8815 Pic+maalim+seif TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pemba. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi kisiwani Pemba kuyatunza na kuyaenzi mafundisho ya Ramadhan.

Maalim Seif alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipojumuika katika futari na baadhi ya wananchi wa kisiwani hapa, aliyowaandalia nyumbani kwake Jadida, Wete.

Alisema Ramadhan ni mwezi wa kipekee wenye kutoa mafunzo kwa wananchi, hivyo ni vyema wakayaendeleza kwa lengo la kujiwekea mazingira bora mbele ya Mwenyezi Mungu.

Alisema kila mmoja anapaswa kutambua kuwa dunia ni sehemu ya mapito, hivyo kuna haja ya binadamu kuendeleza mema kwa ajili ya kesho yao.

Awali, Maalim Seif aliwatembelea wagonjwa na wafiwa mkoani Kusini Pemba akiwataka kuwa na subira na uvumilivu.

Naye mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Wete, Khalifa Mohamed Issa alisema ushirikiano wa wananchi maeneo mbalimbali ni wa kupigiwa mfano.

Issa ambaye ni mbunge wa Mtambwe, aliwataka wananchi kuendelea kumuamini na kukiamini chama hicho. Alisema hakuna haki inayoshindwa daima, bali kilichopo ni muda tu.

Baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kutembelewa na kiongozi huyo wa juu wa CUF, walieleza kufurahishwa na kitendo hicho.

Mwaka Juma, mkazi wa Shehia ya Kojani mkoani Kaskazini Pemba alisema ziara ya Maalim Seif imewapa faraja. “Maalim Seif yupo kwenye nyoyo zetu kwa miaka mingi, ikitokea kumuona basi tunafarijika,” alisema Mwaka.

Chanzo: mwananchi.co.tz