Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maadhimisho Krismasi kitaifa kufanyika Mwanza

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati zikiwa zimesalia siku sita tu kuelekea Sikukuu ya Krismasi, maadhimisho ya Sikukuu hiyo Kitaifa yatafanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) iliyotolewa na Mratibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano, Pascal Mwanache imesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na mkesha wa Krismasi utakaofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Bugando.

Misa ya mkesha itaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda ambaye pia ni msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande.

“Aidha misa takatifu ya Krismasi Desemba 25, 2018 itakayoanza saa nne kamili asubuhi itafanyika katika kanisa la Epifania Bugando na pia itaongozwa na Askofu Renatus Nkwande,” imesema taarifa hiyo.

Baraza hilo limewaalika waumini wa dini hiyo kuungana katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambaye ni mkombozi wa ulimwengu.

Kila ifikapo, Desemba 25 kila mwaka waumini wa dini ya kikristo duniani kote huungana katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambaye kwa mujibu wa dini hiyo ni mkombozi wa ulimwengu.



Chanzo: mwananchi.co.tz