Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MASHINDANO YA KUHIFADH QUR-AN YASHIKA KASI

SHEHE MKUU DAR?fit=1024%2C751 MASHINDANO YA KUHIFADH QUR-AN YASHIKA KASI

Thu, 8 Apr 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Kamati inayosimamia Mashindano  ya Kuhifadhi Qur- an inayoongozwa na Al Had Mussa Salum ambae pia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salam amesema katika fainali hiyo kutakua na makundi manne ikiewemo Kundi la Juzuu ya 3, 7,20 na Juzuu 30 ambapo washiriki wanatarajiwa kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi  miaka 19.

Ameyasema hayo huko Ofisi ya Mufti Mazizini wakati akizungumza na waandishi wa Habari amesema  Washiriki wa Juzuu ya tatu wanatarajiwa kuwa na umri wa mwaka mmoja hadi miaka 9,  na washiriki wa  Juzuu 7 ni kuanzia mwaka moja hadiMiaka 11, na  kwaupande wa juzuu ya 7 ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka 12,  na kwaupande wa juzuu 20 ni kuanzia mwaka mmoja hadi 12.

Pia amesema washiriki wa juzuu 30 ni kuanzia mwaka mmoja hadi 19 ambapo kwasasa Kamati imeeleza kuwa  kumebakia mchujo wa juzuu 30 na  mchujo huo unatarajiwa kufanyika Aprili 9,2021 katika  Masjid Azizi Mtoni kwa Azizi Ally Temeke Dar es Salam.

Mchujo mwengine unatarajiwa kufanyika Masjid Nour Muhammad huko Kiembe Samaki kuanzia tarehe 10,4, 2021 na kumalizika tarehe 18, 2021.

Nchi ambazo zinazotarajiwa kushiriki Mashindano hayo ya Qur -an Kenya, Uganda, Tanzania Bara, Comoro, Sudan. Rwanda, Msumbiji, Burundi, Somalia , Djibout,  Zanzibar na Ethiopia.

Chanzo: zanzibar24.co.tz