Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAHUBIRI YA JUMAPILI: Unavyoweza kupona kupitia damu ya Yesu-2

Sun, 13 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Jina langu naitwa Mtume Dk Peter Nyaga kutoka Kanisa la RGC- Miracle Center Tabata-Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita tuliongelea kuhusu nguvu ya damu ya Yesu katika maisha yako na hatukumaliza.

Leo tuendelee kuitazama hii damu ya Yesu tukiangalia siri za Damu ya Yesu.

Ukweli ni kwamba ukizijua siri hizi na kuamini, utabadilisha maisha yako.

Neno la Mungu limeandikwa kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Yesu alipigwa na kuwekwa msalabani akatoa damu, ili sisi tupone.

Tusome Biblia kitabu cha 1Petro 18-19 imeandikwa ‘Ninyi mfahamu kwamba mlikombolewa sio kwa vitu vinavyoharibika, kwa fedha wala dhahabu mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa, mliopokea kutoka kwa baba zenu bali kwa damu ya thamani kama damu ya mwanakondoo asiye na hila wala waa yaani Kristo.

Namba moja, Biblia imeandikwa wazi kwamba tulikombolewa kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo.

Nataka kuzungumza na wewe kuhusu siri za damu hii. Siri hizo ni maeneo mbalimbali ambayo damu yake ilitoka wakati aliposulubishwa msalabani. Maeneo hayo yanayo tafsiri kubwa katika ulimwengu war oho.

Eneo la kwanza, Yesu alitobolewa mikono yake kwa kipigwa misumari wakati alipowambwa msalabani. Kuna damu ilitoka kwenye mikono ya Yesu, damu ile inasiri kubwa ya ukombozi wa kazi za mikono yetu.

Yaano damu ile kumwagika kwenye viganja vya mikono inafanya kazi ya kukomboa kazi za mikono yetu ili kwa kila unachokifanya, ufanikiwe.

Biblia imeandikwa kuwa ‘atabariki kazi za mikono yetu’ hii inamaana kwamba, damu hiyo imeachilia ukombozi wa kazi hizo.

Siri ya pili ni ile damu iliyotoka kwenye mbavu zake wakati alipochomwa na mkuki. Hii ina maanisha ukombozi wa uzao wa tumbo la mwanamke. Kwa sababu mwanamke alitoka kwenye mbavu za mwanaume kwa hiyo Yesu alitobolewa mbavu ili akomboe uzao wa mwanamke.

Siri ya tatu ni ile damu iliyotobolewa kwenye miguu ambayo ilikuwa inaashiria umiliki wa ardhi.

Unajua wakati mwanadamu wa kwanza alipotenda dhambi alipokonywa umiliki wa ardhi kwa hiyo, damu ilipomwagika miguuni iliweza kurejesha umiliki huu.

Katika kitabu cha Joshua 1:3 imeandikwa kwamba mahali popote ambapo nyayo za miguu yako zitakanyaga nimewapa umikili na utawala.

Damu nyingine ni ile iliyotoka kichwani. Miiba katika biblia inatafsiri laana hii ina maana kuwa ile damu iliyotoka kichwani ilikuwa inatafsiri kufuta na kuondoa laana zetu.

Msomaji wa Mwananchi nikuombee kabisa kama kuna laana yoyote inakufuatilia ifutwe kwa damu ya Yesu.

Kama hujawahi miliki chochote, Mungu akupatie umiliki wako na ninatamka ukombozi wa uzao wa tumbo la mwanamke. Kama unafanya kazi lakini mikono yako haizalishi, kama neno la Mungu linavyosema utabarikiwa kwa kazi za mikono yako nakuombea ikawe hivyo.

Kuna damu nyingine ya agano ilitokana na kutahiriwa, hii pia inayo maana kubwa, kwa hiyo popote ilipotoka ilikuwa na maana, nguvu na kurejesha maisha yetu tena.

Mambo ambayo yanaweza kurejeshwa na damu ya Yesu ni pamoja na uwezo wa kufikiri, akili na ufahamu.

Kuna watu walikuwa na akili kubwa za maisha ikiwamo biashara lakini ziliibiwa kwa sababu mbalimbali Mungu akarejeshe upya.

Yhana 10:10 inasema hivi, alikuja kuua, kuiba, kuharibu ila Yesu alikuja tuwe na uzima tele. Hii ina maana kuwa Yesu aliteswa msalabani ili kukurejeshea kile kilichoibiwa.

Mungu akurejeshee kila ulichoibiwa na mwizi, ili mwaka huu 2019 Mungu atende mambo makubwa zaidi kwenye maisha yako. Kwa sababu Yesu anaitwa ufufuo na uzima, amini kwamba kila unalopitia damu ya Yesu inaweza kulibadilisha.

Hata kama unateseka kwenye magonjwa bado damu hii ya thamani ina uwezo wa kukuponya.

Tumeokoka kwa sababu damu hii imefanikiwa kurejesha mambo magumu ambayo kwa akili zetu yalikuwa hayawezekani kabisa.

Huenda unapita kwenye mambo magumu zaidi, laana, mikosi na balaa amini kwamba mateso hayo yanaweza kuisha kabisa ikiwa utaruhusu na utakubali kumwamini Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wako.

Ndugu msomaji wa Mwananchi, unaweza kuitumia damu hii itende kwenye maisha yako ukiamini. Omba rehema kwa Mungu kwa sababu anasamehe dhambi.



Chanzo: mwananchi.co.tz