Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAHUBIRI YA JUMAPILI: Kufunguliwa ufahamu na onyo kwa wakristo kuhusu alama za utambulisho wa shetani

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mada ya leo inaongozwa na kichwa kinachosema kwamba ‘Kufunguliwa ufahamu na onyo kwa wakristo kuhusu alama za utambulisho za kishetani’.

Katika somo hili tunongozwa na neno la Mungu kutoka kwenye biblia kitabu cha Matendo 19:19.

Neno la Mungu limeandikwa kwamba; “Na watu katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.”

Katika maisha yetu ya kawaida kuna watu ambao hupenda kuchora michoro kwenye miili yao inayoitwa ‘tattoo’.

Watu wengi wameathirika na alama hizi za kishetani kwa kujua na kwa kutokujua.

Ukweli ni kwamba wengi wanaochora hii michoro hawajui maana halisi ya michoro yao.

Pia Soma

Huduma ya uponyaji wa Kimasihi iliyofanywa na Petro na Yohana iliendelea hata kwa Paulo.

Baadhi ya waganga wa Kiyahudi waliotembela sehemu mbalimbali, walivutiwa sana walipomwona Paulo akitoa pepo wachafu kwa Jina la Yesu, wakajaribu kuiga mambo hayo lakini wakashambuliwa vibaya sana na mashetani.

Mambo ya kupiga bao na uchawi yalienea sana sehemu za Efeso, lakini Mungu alifanya kazi yake kwa nguvu na mamlaka makubwa na watu wengi waliamini.

Uponyaji wa watu unatakiwa kimwili, kiroho na hata kiakili.

Katika dunia ya leo watu wanasumbuliwa na uovu wa kishetani kupitia alama wanazozitumia pasipo wao wenyewe kujua kama hizo ndizo zinawasumbua na nyingine zipo kwenye bidhaa wanazotumia.

Huu ni utumwa unaoitesa jamii kubwa. Alama hizi huitafuna dunia na kuleta utumwa kwa watumiaji.

Jiulize; ipo migogoro mingi kwenye familia? Kanisa? vyama vya siasa? na kwingine kwingi.

Pia jiulize je nchi yako imedumaa kiuchumi? Kwa nini watu hawapatani?

Ukweli ni kwamba alama za kishetani zinaweza kutumika kwa njia ya mawasiliano.

Tena hasa kwa kutumia mikono kwani wahusika hutambuana kwa njia hiyo.

Viongozi wa ngazi za juu, kisiasa, kiserikali na hasa katika mataifa makubwa, picha za mitandaoni zinaonyesha matumizi ya alama hizi wakati wanasalimiana.

Sio kwamba wanaigiza bali ni utambulisho wa kikundi au jamii ambayo mambo yao yanafahamika na kukubalika na mkuu wa ufalme wao.

Mashoga wanaweza kufahamiana kwa alama zao vivyo hivyo kwa wasagani.

Ukristo sio falsafa fulani kwamba ulianzia Palestina, ukaenea Ugiriki ukawa falsafa, ukaenea hadi Rumi ukawa taasisi, ukaenea Ulaya ukawa utamaduni, ukafika Amerika ukawa shughuli kama biashara vile hapana, Ukristo sio biashara.

Ajenda iliyopo leo duniani inayoendeshwa kwa siri kubwa kwa kutumia alama hizi za kishetani ni kumtawala mwanadamu kiuchumi.

Kazi hii inafanyika kupitia alama, pesa na hata siasa kwa sababu taasisi kubwa za kidunia hutumika pia kuzitawala nchi changa .

Leo Mungu nakupa ufahamu huu mpya. “Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza na kuomba, na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao,” huu ni mstari kutoka katika kitabu cha 2 Nyakati 7:14.

Pia Mathayo 13, kuna mfano wa ngano na magugu.

Neno la Mungu linasema lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika bonde lako? Limepata wapi basi magugu?

Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, basi wataka twende tukayakusanye?

Akasema, La; msije mkakusanya magugu na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno.

Tujinyenyekeze mbele za Mungu na huko ndiko kuna uzima.

Tunaweza shinda alama hizi za shetani na mbinu zake kwa kumwamini na kumpokea Yesu ili awe mwokozi kwenye maisha yetu.

Chanzo: mwananchi.co.tz