Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lusekelo, Gwajima, Mwingira waungana na Magufuli Ikulu

31269 Viongozipic TanzaniaWeb

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo leo Jumatano Desemba 12, 2018 wameungana na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Leo Rais Magufuli anasaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Pori la Akiba la Selous wa Stiegler’s Gorge na viongozi hao wa dini wamekuwa miongoni wa viongozi mbalimbali wa dini waliohudhuria hafla hiyo.

Kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, viongozi hao wa dini walianza kwa kufanya maombi kila mmoja, kuwa vivutio miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir, Askofu Mkuu  wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Mahimbo Mndolwa,

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz