Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lugha ya alama kwa viziwi kuzinduliwa

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua  usanifishaji wa lugha ya alama nchini katika kilele cha maadhimisho ya wiki la viziwi yatakayofanika kitaifa mkoani Iringa.

Akizungumza leo Ijumaa Septemba 27, 2019 mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita), Nidrosy Mlawa amesema Serikali imeamua kuzindua lugha ya alama ili kuwasaidia wanafunzi viziwi katika elimu.

Amesema mradi huo utatekelezwa chini ya Wizara ya Elimu kupitia taasisi ya elimu Tanzania na matarajio yao lugha ya alama itafundishwa kama somo darasani.

"Kukosekana kwa lugha ya alama  nchini kumeathiri  maendeleo ya viziwi hasa katika elimu kwa sababu matokeo ya watoto viziwi katika shule nyingi ni mabaya, ni kutokana na kukosekana kwa lugha ya alama shuleni,” amesema Mlawa.

Mwalimu wa shule ya viziwi Iringa,  Godfrey Mbwilo amesema  matokeo ya shule ya viziwi Njombe yalikuwa mabaya hivyo kuzinduliwa kwa alama hizo kutasaidia kuondoa changamoto mbalimbali.

“Lugha hii ya alama Tanzania ikianza kufundishwa shuleni jamii pamoja na viziwi wataweza kuwasiliana na kuelewana na kuzungumza lugha moja jambo ambalo litawasaidia kupata maendeleo pamoja na huduma nyingine  muhimu.”

Pia Soma

Advertisement

“Kuna viziwi wengi wanakwama kupata taarifa lakini jamii inapaswa itambue kuwa wanao uwezo mkubwa wa kufanya kazi na kupata maendeleo kama watu wengine hivyo wanahitaji ushirikianao hasa katika mawasiliano,” amesema Mbwilo.

Katibu wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Iringa,  Shaib Juma amesema Chavita wanachohitaji ni watu kujifunza lugha ya alama ili  iweze kutumika nchini kote kama ilivyo lugha ya Kiswahili.

“Tunacholenga ni watu wajifunze lugha ya alama ili mimi kiziwi ninapokutana na mtu yeyote tuweze kuwasiliana bila kikwazo.”

“Jamii inapokuwa imejifunza watu wote tunakuwa na maelewano sawa, tofauti na ilivyo sasa kiziwi ninapokutana na mtu ambaye hajui lugha ya alama kuwasiliana inakuwa changamoto,” amesema Shaib.

Chanzo: mwananchi.co.tz