Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lowassa, Gondwe washiriki ibada ya mazishi ya mtoto wa Mwakasege

22568 Lowassa+pic TanzaniaWeb

Wed, 17 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na  Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ni kati ya waombolezaji walioshiriki ibada ya mazishi ya Joshua Mwakasege, mtoto wa mwalimu Christopher Mwakasege.

Joshua alifariki dunia Octoba 11, 2018 katika Hospitali ya Agha Khan baada ya kuugua ghafla wakati akiwa kazini.

Ibada ya mazishi imeanza saa 8 mchana katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Mbezi Beach.

Kabla ya ibada kuanza, waombolezaji walianza kutoa heshima za mwisho.

Mwili wa Joshua ambaye ni mtoto pekee wa kiume mwalimu Mwakasege, utasafirishwa kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya kwa maziko.

Chanzo: mwananchi.co.tz