Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kongamano la amani kufanyika Dar Septemba 7

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika lisilo la kiserikali la kupigania amani ulimwengni (HWPL) limeandaa kongamamo la kimataifa la amani ambalo limepangwa kufanyika Septemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa Mbudya, Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa kongamano hilo nchini Danice's Coworker imeeleza kongamano hilo litafanyika Septemba 7 mwaka huu na litahudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya Amani.

Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na mpango maalum wa kuhakikisha amani inakuwepo  ambapo viongozi mbalimbali wa dini, viongozi wa wanawake, watoto na viongozi wa vyama vya siasa pamoja na waandishi wa habari wamealikwa.

Taarifa hiyo ilisema mwaka huu HWPL imeamua kufanya kongamano hilo kwa njia ya pekee kwa sababu kila nchi itashirikishwa katika eneo lake tofauti na miaka mingine ambapo huchagua nchi moja na kufanya ambapo mwaka jana lilifanyika nchini Afrika Kusini.

Katika kongamano hilo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kuzishauri nchi mbalimbali ambazo hazijasaini mikataba ya amani duniani kusaini, kufundisha umuhimu wa amani na madhara ya amani inapopotea.

Kongamano hilo ambalo ni la 5 kufanyika tangu lilipoanzishwa limepangwa kufanyika katika maeneo zaidi ya 150 na kushiriksha nchi 110, baadhi ya nchi hizo ni Korea Kusini, Ufaransa, Australia, Urusi, India, Zambia na Marekani.

Pia Soma

Advertisement


Chanzo: mwananchi.co.tz