Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitabu cha zamani zaidi cha Kikristo kuuzwa

Kitabu Cha Zamani Zaidi Cha Kikristo Kuuzwa Kitabu cha zamani zaidi cha Kikristo kuuzwa

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Kitabu cha zamani zaidi cha dini ya Ukristo, kulingana na jumba la mnada la Christie's, kitauzwa mwezi Juni.

Kodeksi ya Crosby-Schøyen, iliyoandikwa kwa hati ya Kikoptiki kwenye mafunjo nchini Misri, ni ya kati ya 250-350AD.

Pia kinafikiriwa kuwa mojawapo ya vitabu vya zamani zaidi vilivyopo na kinaweza kuuzwa hadi $3.8m (£3m).

Kitabu cha kiliturujia kilitolewa katika mojawapo ya monasteri za kwanza za Kikristo na kina maandishi kamili ya vitabu viwili vya Biblia.

Maandishi hayo ni ya "umuhimu mkubwa kama shahidi wa kuenea kwa mapema zaidi kwa Ukristo katika eneo la Mediterania," alisema Eugenio Donadoni, mtaalamu mkuu wa vitabu na hati katika Christies.

"Watawa wa kwanza kabisa katika Misri ya Juu katika makao ya watawa ya Kikristo ya kwanza walikuwa wakitumia kitabu hiki kusherehekea sherehe za mapema zaidi za Pasaka, miaka mia chache tu baada ya Kristo na miaka mia moja au zaidi baada ya Injili ya mwisho kuandikwa."

Kitabu hiki ni sehemu ya Bodmer Papyri, mkusanyiko wa maandishi kadhaa ambayo yaligunduliwa katika miaka ya 1950, na yanajumuisha maandishi ya Kikristo, dondoo za Biblia na fasihi za kipagani.

Chanzo: Bbc