Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis awasili nchini Sudan Kusini

Kiongozi Wa Kanisa Katoliki Papa Francis Awasili Nchini Sudan Kusini Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis awasili nchini Sudan Kusini

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Papa Francis amewasili katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, ambapo ataanza misheni ya kihistoria ya amani na viongozi wawili wa kanisa la Uingereza.

Mpango wake wa pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland ni wa kipekee kwa wanakanisa hao watatu.

Papa Francis anaheshimu ahadi ya 2019 ya kuzuru Sudan Kusini, wakati katika ishara ya kushangaza ya amani alibusu miguu ya viongozi wa makundi hasimu ya nchi hiyo huko Vatican.

Ziara hiyo ya Juba inajiri siku moja baada ya ripoti kuwa watu ishirini na saba waliuawa katika ghasia katika jimbo la Equatorial ya Kati .

Kulingana na Mwandishi wa BBC Mercy JUMA anayeripoti kutoka Juba, mitaa ya Juba tayari ilikuwa imejaa maelfu ya watu waliokaidi joto kali na kumsubiri Papa Francis ambapo wengi walionekana kuimba , kucheza desni na kupeperusha bendera ndogo, zenye sura ya Papa.

Watu wengi ambao BBC ilizungumza nao wana matumaini kwamba ziara hii itageuza hali katika nchihiyo iliyoathiriwa sana na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.

Sudan Kusini imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ukosefu wa utulivu wa kisiasa tangu ilipojipatia uhuru wake mwaka 2011 baada ya mapambano ya kisiasa kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wa rais wa wakati huo Riek Machar, mzozo ambao umegharimu maisha ya watu 400,000 na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Mwaka 2019 Papa alibusu miguu ya viongozi hao wawili walipokutana mjini Vatican katika juhudi za kuhimiza amani - kitendo ambacho kiliwashangaza wengi. Lakini leo, viongozi wa sehemu tatu tofauti za kanisa la Kikristo watakuwa nchini, pamoja, kwa wakati mmoja.

Chanzo: Bbc