Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikwete, Dk Bashiru washiriki ibada kuagwa Balozi Kaduma

74005 Msibapic

Tue, 3 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ni kati ya viongozi waliopo katika  ibada ya kuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Balozi Ibrahim Kaduma.

Ibada ya kwanza ya kuaga mwili wa waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje imeanza leo asubuhi Septemba 3, 2019 nyumbani kwake Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

Ibada nyingine inatarajia kufanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Makongo Juu.

Yohana Kaduma amesema mwili wa baba yake utasafirishwa Alhamisi kuelekea nyumbani kwake Kibena Mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.

Balozi Kaduma (82) alifariki dunia akiwa nchini India alikoenda kwa ajili ya matibabu.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement   ?

Chanzo: mwananchi.co.tz