Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana wa Misri ajinyakulia mamilioni mashindano ya Qur’an Tanzania

Kijana Wa Misri Ajinyakulia Mamilioni Mashindano Ya Quran Kijana wa Misri ajinyakulia mamilioni mashindano ya Qur’an Tanzania

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Raia wa Misri Omar Mohammad Hussein ameibuka kidedea katika mashindano ya Afrika ya kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo.

Hussein amewashinda washiriki wenzake 23 kutoka nchi 23ndani na nje ya bara la Afrika na kujizolea zawadi ya shilingi milioni 23 ambazo ni sawa na dola elfu 10 za kimarekani.

Wakati huo huo, watanzania wawili ambao wameweza kuibuka katika tano bora ni Adurahim Abubakar Masoud, ambae ameshika nafasi ya tatu na Bakari Juma Hamadi nafasi ya tano.

Mashindano hayo ya 23 yameshuhudiwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya nchi.

Chanzo: Bbc