Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Askofu Dr. Shoo kuhusu Ndugai Kujiuzulu

Ndugai?fit=539%2C343&ssl=1 Alichokisema Askofu Dr. Shoo kuhusu Ndugai Kujiuzulu

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Glorious Shoo amesema kujiuzulu kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ni aibu kwa Taifa.

Dk Shoo, ambaye ni mchungaji kiongozi wa Kanisa la Kilimanjaro International Christian Centre (KICC), alisema wapo watu wanaoshangilia kujiuzulu kwake wakidhani ni malipo ya udhalimu wa kutotenda haki, lakini yapo mambo ya kujifunza, ikiwamo kutenda haki.

Askofu Shoo alisema hayo jana ,wakati akizungumza na Mwananchi ofisini kwake, huku akiwaomba wanaopewa dhamana na mamlaka ya kulitumikia Taifa kutenda haki.

“Kwenye jambo ambalo la kujifunza ni suala la haki, haki huliinua Taifa, tunapoona matendo yasiyo ya haki yanayofanywa na baadhi ya watu ambao wamepewa mamlaka na madaraka ya kuyatumia vibaya halafu tukashangilia, huo sio Utanzania tuliouzoea,” alisema Askofu Shoo.

“Wako watu wengi wanaoshangilia kwa sababu wanahesabu ni malipo ya udhalimu ya kutokutenda haki, lakini hii ni aibu kwetu sote.

Advertisement “Hii ni aibu yetu, tumefika tulikofika na ni kweli inasikitisha, kuwa watu wanaweza kushangilia na kufurahia anguko la mtu mwingine, tukifikia hapo ni mahali pabaya kwa Taifa, haijalishi ya kwamba kweli mtu analipwa kulingana na matendo yake, lakini sio afya kufurahia maumivu ya mtu mwingine,” alisema Askofu Shoo na kuongeza:

“Jambo la kujifunza turudi kama Taifa lilivyokuwa, tukiitana ndugu na tulisaidiana lakini sicho kinachoendelea kwa sasa hivi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live