Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katoliki wasema tozo ni kikwazo uendeshaji wa shule zao

Katoliki Pc Data Katoliki wasema tozo ni kikwazo uendeshaji wa shule zao

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Umoja wa Mapadre wa Kanisa Jimbo Katoliki Moshi (UMAWATA) wameiomba Serikali kupunguza ama kuondoa kabisa baadhi ya tozo na kodi ambazo zimekuwa kikwazo katika uendeshaji wa shule.

Wamesema kumekuwa na changamoto kwa shule zinazosimamiswa na Umoja huo kutokana na tozo na kodi hizo hivyo, zikiondolewa itasaidia kushiriki jitihada za Serikali kuboresha utoaji wa elimu bora nchini.

Ombi hilo limetolewa Jumapili ya Oktoba 24, 2021 katika ibada takatifu ya kuwaombea wanafunzi wa kidato cha nne iliyofanyika katika Sekondari ya Mtakatifu, Papa Yohani Paulo wa Pili, Lombeta wilayani Moshi, Kilimanjaro.

Ibada hiyo imekwenda sambamba na sherehe za mahafali ya 43 ya shule hiyo. Akizungumza katika ibada hiyo, Padre Dk Aidan Msafiri amesema Serikali iweke utaratibu maalumu wa kuziwezesha shule zinazomilikiwa na taasisi za kidini kwa kuondoa kodi na tozo kwa sababu wamekuwa wakitoa huduma kwa jamii.

"Shule zetu zinazoendeshwa na mapadre haziko kibiashara bali zinatoa huduma kwa jamii na wale wanoishi katika mazingira magumu, lakini Serikali inazitoza kodi na tozo mbalimbali hatua ambayo inazifanya zishindwe kujiendesha na nyingine zimefungwa," amesema Padre Msafiri.

Pia, ametumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi wanaojiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne kumwamini Mungu kwa kuwa ndiye mkuu kwa kila jambo.

Mwenyekiti wa Bodi ya UMAWATA, Padre Faustine Furaha, ameiomba Serikali kuangalia namna ya kutofautisha shule zinazofanya biashara na zile ambazo zinatoa huduma kwa jamii kuweka mpangilio sahihi wa ulipaji tozo na kodi.

"Shule zetu hazifanyi biashara tunatoa huduma hivyo, Serikali itofautishe kati ya zinazofanya biashara na zile ambazo hatufanyi biashara. Shule za Katoliki zinatoa huduma na sio biashara," amesema Padre Furaha.

Naye Mkuu wa Shule hiyo Padre Cleophas Bossi, amesema uwepo kwa kodi katika shule zinazomilikiwa na mapadri ni pigo kubwa kwa jamii kwani, kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kujiendesha na kufikia malengo ya utoaji elimu bora.

Chanzo: mwananchidigital