Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Bakwata Morogoro afurushwa

Town Baraza Mkoa halikuanisha wala kutoa maelezo zaidi

Thu, 27 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Baraza Kuu la Waisilam Tanzania BAKWATA Mkoa wa Morogoro imemsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Baraza hilo Mkoa wa Morogoro Ustadhi Ahmad Heirallah kutokana na ukiukwaji wa maadili ya uongozi.

Taarifa ya kusimamishwa kazi kiongozi huyo imetolewa na Kaimu Sheikhe Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Morogoro Sheikh Twaha Kilango baada ya kikao cha baraza la mashekhe Mkoa wa Morogoro.

Aidha amesema baraza halitomvumilia na kusita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayekiuka maadali ya uongozi wa dini hiyo na kuwataka waumini kuwa na imani na viongozi wao.

Hata hivyo Sheikh Kilango amesema Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Morogoro imemteua Ustadhi Muhammad Bafadhwili kukaimu nafasi hiyo hadi taratibu za kumpata katibu zitakapokamilika.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo kaimu katibu wa BAKWATA Mkoa wa Morogoro Ustadhi Muhammad Bafadhwili amelishukuru baraza hilo kwa kumuamini na kumchagua kushika nafasi hiyo na kuwaongoza waislam wanzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live