Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kardinali Pengo awaomba Uwaka watimize wajibu wao

22292 PENGO+PIC TanzaniaWeb

Mon, 15 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amewataka Uwaka kumwomba Mungu awawezeshe kutimiza wajibu wao kwenye familia na katika nafasi za kiuongozi walizonazo.

Kardinali Pengo ameyasema hayo leo katika mahubiri yake kwenye maadhimisho ya misa takatifu iliyowakutanisha wanaume Wakatoliki wa Jimbo la Dar es salaam, iliyofanyika kituo cha wadada wadogo (masista) Visiga mkoa wa Pwani.

Amesema lengo kubwa la kufanya misa hiyo ni kutoa shukrani kwa Mungu hasa wakati huu kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya uinjilishaji hapa nchini yanayotegemewa kuanza Novemba 2 hadi 4 Bagamoyo mkoani Pwani.

Amesema miaka 150 iliyopita kabla wamisionari hawajaingia nchini kulikuwa hakuna thamani kabisa kwani watu walikuwa wanachinjwa kama ng’ombe au mbwa na kupigwa kama wanyama.

“Tulikuwa hatuna thamani yoyote, tunachinjwa kama nguruwe ndio ilikuwa hali yetu mnauzwa kama nguruwe au mbwa,” amesema Kardinali Pengo

Akimtolea mfano binti aliyekuwa anaitwa Siwema ambaye wazazi wake wote waliuwa wakati huo wa utumwa na yeye kutupwa pamoja na wafu hadi aliookotwa na wamisionari akajengewa imani ya Kikristo na kuwa mfano kwa wengine katika kumtangaza Kristo.

“Sana sana unaweza kusema kosa lake lilikuwa nini hadi kupelekea kutupwa pamoja na wafu au ni kwa sababu ya kuzaliwa Tanzania, tulijihesabu kama watu wenye mkosi wakati huo.”

“Sisi watu wa Tanzania na Afrika kwa jumla tunaambiwa twende kwa ndugu zetu tukawaeleze matendo makuu ya Mungu aliyotutendea kwa kutufanya leo hii injili inahubiriwa kila mahali kwa uhuru bila kuuzwa wala kuchinjwa kama ilivyokuwa miaka hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz