Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kardinali Pengo atoa nasaha kwa waumini

44622 Pic+pengo Kardinali Pengo atoa nasaha kwa waumini

Mon, 4 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewatia moyo Wakristo nchini, akisema iko faida nyingine zaidi katika uendeshaji wa Kituo cha Tumaini Media.

Kardinali Pengo amesema katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, kanisa hilo halijawahi kupata mabilioni ya fedha yanayotokana na mradi huo, lakini ndani ya moyo mtakatifu wa Yesu, waumini wa kanisa hilo hawatakiwi kuhesabu hasara ila kinyume chake.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa misa ya kuadhimisha miaka 25 ya Radio Tumaini, iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu Joseph- Posta jijini Dar es Salaam.

Katika risala yao wafanyakazi wa kituo hicho waliwashukuru maparoko, mapadre, watawa wa kike na kiume, vyama vya kitume na marafiki wa chombo hicho kwa ushirikiano na utayari wa kukosoa, kushauri na kuchangia gharama za uendeshaji wa kituo hicho.

“Ni kukosa busara kuanzisha chombo kama Tumaini na vingine vyote vya Tumaini media katika mahitaji makubwa ya fedha ulimwengu wa leo? Je ni upumbavu?” Alihoji Kardinali Pengo.



Chanzo: mwananchi.co.tz