Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa lawataka viongozi kuacha siasa kuhusu corona

100246 Makanisa+pic Kanisa lawataka viongozi kuacha siasa kuhusu corona

Fri, 27 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Katibu Mkuu Kiongozi wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Mchungaji Josephales Mtebe amewataka wanasiasa nchini Tanzania kutoingiza itikadi za vyama vyao katika vita dhidi ya virusi vya corona, badala yake waunganishe Watanzania pamoja kukabiliana na janga hilo la Kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Jumatano Machi 25, 2020, Mchungaji Mrebe amewataka viongozi hao kuepuka kutoa kauli zenye lengo la kuwabeza wenzao wala kuwagawa Watanzania katika misingi ya itikadi za vyama  katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

“Mapambano dhidi ya virusi vya corona yatuunganishe wote bila kujali tofauti za itikadi na dini zetu, kila Mtanzania kwa nafasi yake awe sehemu ya vita hivyo,” amesema.

Kuhusu mikakati ya kanisa hilo kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, amesema kanisa limesitisha mialiko na safari zote za kwaya na wahubiri kutoka kanisa moja kwenda nyingine wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.

“Ili kuepuka mikusanyiko mikubwa ambayo imekuwa sehemu ya ya utamaduni wa kanisa letu kwa miaka mingi, mikutano ya Pasaka itaadhimishwa katika makanisa yetu ya mitaa.”

 

Pia Soma

Advertisement
“Ni muhimu waumini, wachungaji na viongozi wote wa kanisa kuzingatia maelekezo ya tahadhari na kanuni ya afya ya kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka, kutosalimiana kwa mikono kabla na baada ya ibada, kutokuwa na ibada ndefu na kuwa na uangalizi wa karibu wa watoto wakati wa ibada,” amesema.

Constantine Mkandya ambaye ni mchungaji wa Kanisa Kuu la AICT Makongoro ya jijini Mwanza ameishukuru Serikali kwa kuruhusu shughuli za ibada kuendelea huku aiwahimiza Watanzania kila moja kwa imani yake kumshirikisha Mungu katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Amesema kuanzia ibada ya Jumapili iliyopita, kanisa lake inatekeleza maelekezo ya kuweka vifaa na maeneo maalum ya kila muumini kunawa mikono kabla na baada ya kutoka ibadani.

“Wazee wa kanisa pia wanasimamia maelekezo ya kuhakikisha waumini hawakai kwa kubanana wakati wa ibada; yote hii ni kushiriki vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona,” amesema mchungaji Mkandya

 

Chanzo: mwananchi.co.tz