Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa la Vosh latoa salamu za pole kwa Watanzania

A4fa04e27d29b04b61a4626ff4883df8.png Kanisa la Vosh latoa salamu za pole kwa Watanzania

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIONGOZI wa Kanisa la Vosh International, Dk Winnie Owiti mkazi wa Nairobi nchini Kenya ametuma salaamu za pole kwa Watanzania kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya Owiti, Makamu Askofu mkuu kiongozi wa kanisa hilo, Mchungahi Joseph Mtatiro alisema salamu za pole wanaomba ziwaifikie Rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mke wa Magufuli Janeth na watoto wake wote na familia yote kwa ujumla.

"Kwa niaba ya makanisa ya Vosh International yaliyopo nchini Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi tunaeleza wazi kuwa tunamtambua Magufuli katika uhai wake hakuwa na hata chembe ya ubaguzi wa kidini," alisema.

Alisema pia kiongozi huyo alijitoa kwa moyo wake wote na kwa nia njema katika kulitumikia taifa, kiasi ambacho kiliwezesha nchi kuingia kwenye uchumi wa kati.

Ujenzi wa miradi mikubwa unaoendelea nchini na mingine iliyokamilishwa katika kipindi kisichozidi miaka mitano ya uongozi wake, ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa na kiongozi huyo wa kiroho kuwa yanadhibiti nia njema aliyokuwa nayo Rais Magufuli kwa taifa.

"Kanisa la Vosh katika Afrika Mashariki na Kati lilimpenda na kumheshimu sana kwa jinsi alivyomheshimu Mungu na alivyokuwa mhudhuriaji mzuri wa ibada," alisema Mtatiro

Alisema, Magufuli katika uhai wake aliheshimu dini zote kubwa kwa ndogo na hivyo uhuru wa kuabudu ukawa na wigo mpana hali iliyosababisha kutokuwepo misigano ya kidini katika kipindi chote cha uongozi wake.

Zaidi ya yote hayo, Mtatiro alisema kiongozi huyo ameacha historia ya tofauti kwani hakujihusisha na kufanya biashara kwa maslahi yake binafsi bali mambo mengi aliyoyasimamia kwa nguvu na moyo mkuu ni yenye maslahi kwa umma wa Tanzania.

Alisema imani ya kanisa hilo ni kwamba, mbinguni ni mahali salama na wote wafao katika Bwana Mungu huenda mahali salama.

Chanzo: www.habarileo.co.tz