Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa kuimarisha kiwango cha elimu Shule ya St Monica

692c33a92c7039826e111cead351e84a Kanisa kuimarisha kiwango cha elimu Shule ya St Monica

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Dk Michael Hafidh amesema wamejipanga kuimarisha kiwango cha elimu katika Shule ya St Monica iliyopo Kiungani ili iweze kutoa elimu ya msingi na sekondari kwa kiwango kitakachozalisha wataalamu wa baadaye.

Alisema hayo katika sherehe za mahafali ya wanafunzi wa darasa la sita na kidato cha nne katika shule hiyo iliyopo Kilimani Unguja na kuwa wapo katika mchakato wa kuirudisha shule hiyo jina lake la zamani la Saint Paul Kiungani.

Askofu Hafidh alisema huduma za elimu zimeimarishwa kwa kiwango kikubwa katika shule hiyo ambayo ilianza ya msingi darasa la kwanza na kufikia hatua hadi sekondari kidato cha nne na kuongeza kuwa mafanikio hayo yote yanatokana na ushirikiano wa uongozi wa kanisa pamoja na shule hiyo wakiongozwa na wazazi ambao hufikisha watoto wao shuleni kupata elimu.

Aidha aliwpaongeza walimu wa shule hiyo kwa juhudi zao kubwa na kuvumilia zaidi katika kipindi cha corona ambapo tatizo la fedha ikiwemo mishahara lilijitokeza.

Mapema mkurugenzi wa shule ya Saint Monica, Padri Furaha Nyoka alisema shule imepata mafanikio makubwa na kukubalika katika taasisi za elimu kwa kupanda daraja kutoka shule ya msingi hadi sekondari.

Aidha alisema shule imefanikiwa huku wanafunzi wengi wakifaulu kuingia kidato cha sita katika mitihani ya taifa na kujenga imani kubwa kwa wazazi.

Jumla ya wanafunzi 60 walihitimu katika masomo yao ikiwemo wa kidato cha nne baada ya kufanya mitihani ya taifa katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule kongwe Zanzibar.

Chanzo: habarileo.co.tz