Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa Uganda kuchukua asilimia 25 ya fedha za maombelezo

Tue, 25 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala. Uganda.  Kanisa la Anglikani nchini Uganda limetoa mwongozo mpya ambako sasa itakuwa ikichukua asilimia 25 ya fedha za rambirambi zitakazopatikana katika msiba.

Utaratibu huo mpya uliotangazwa jana June 25 na Katibu wa Dayosisi ya Namirembe jijini Kampala, Padri, Nelson Kaweesa katika barua yake ya June 7.

Barua hiyo inaondoa sintofahamu ambako hivi karibuni vyombo vya habari nchini humo vlliandika kwamba kanisa hilo limetoa mwongozo wa kuchangia asilimia 75 ya fedha za rambirambi na 25 zibaki katika familia.

Kwa mujibu wa Padri Kaweesa, tayari utaratibu huo umewasilishwa katika baraza la dayosisi hiyo na utaanza kutekelezwa.

Kaweesa alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Mei 24 ambako sasa asilimia 25 ya fedha za maombelezo zitakazokuwa zikikusanywa zitabakizwa kanisani ili kusaidia uendeshaji wa kanisa na tayari taarifa hiyo imewasilishwa kwa mkuu wa dayosisi hiyo kwa ajili ya hatua za utekelezaji.

Kwa mujibu wa barua hiyo, fedha hizo zitahusisha shughuli zote za mazishi yatakayofanyika nyumbani au sehemu nyingine yoyote.

Pia Soma

Padri Kaweesa aliandika kwamba “taarifa hiyo inafafanua makosa yaliyofanywa awali ambako ilielezwa kwamba kanisa litachukua asilimi 75 na 25 kwenda kwa familia.

Chanzo: mwananchi.co.tz