Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa Katoliki lafafanua kauli ya Papa

Fri, 8 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vatican.Kanisa Katoliki limeyafafanua leo matamashi ya Papa Francis kuhusu  kile alichokiita kuwa ni utumwa wa ngono katika shirika moja la watawa la kifaransa, likisema kuwa alimaanisha matumizi mabaya ya madaraka ambayo yalionekana katika matukio ya unyanyasaji wa kingono.

Papa Francis amesema hayo akilijibu swali kuhusu unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mapadri dhidi ya watawa wakati wa kikao cha waandishi wa habari aliporejea nyumbani kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ilikuwa ni mara ya kwanza ya kwa Papa Francis kukiri hadharani kuhusu tatizo la mapadre na maaskofu kuwanyanyasa kingono watawa.



Chanzo: mwananchi.co.tz