Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa Katoliki kutuma ujumbe wa Papa Francis kwenda mwezini

Papa Kuhitimisha Ziara Sudan Kusini  Kwa Misa Takatifu.jpeg Papa Francis

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makao makuu ya kanisa katoliki kule Vatican, Italai wametangaza mpango wa kutuma ujumbe wa matumaini wa papa Francis kwenda angani.

Ujumbe huo wa Papa Francis ni ule ambao alionekana akifanya maombi akiwa peke yake katika ukumbi wa Mtakatifu Petro katikati mwa janga la Covid-19 mwaka 2020.

Hotuba ya papa akiomba peke yake katika uwanja tupu wa St Peter’s imegeuzwa kuwa “Kitabu cha nano” chenye upana wa chini ya milimita mbili, ambacho kitazinduliwa na kutumwa mwezini mnamo 10 Juni.

Itasafiri kuzunguka Dunia kwa satelaiti iliyoundwa kimakusudi katika mwinuko wa takriban kilomita 525, ikitumwa kwa roketi ya SpaceX Falcon 9 kutoka Vandenberg Space Force Base huko California, AFP waliripoti.

Mnamo Machi 27, 2020, papa aliwahimiza wafuasi ambao walihisi “kuogopa na kupotea” mbele ya kile ambacho wakati huo kilikuwa virusi vya kutisha kuwa na imani.

Mradi huo sio wa kwanza kwa papa kufanya safari ya anga mwaka wa 2017, alipiga simu ya video na wanaanga kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga cha Juu (ISS), ambapo aliwauliza kuhusu “mahali pa mwanadamu katika ulimwengu”.

Mradi wa “Spei Satellites” gharama na ufadhili wake haujafichuliwa mpaka sasa na unaratibiwa na Shirika la Anga la Italia kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali za Italia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live