Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa KKKT Konde lafungwa, waumini watawanywa

Kaaanisaa Picc Dataa Kanisa KKKT Mbeya lafungwa, waumini watawanywa

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeingilia kati na kutimua maandamano na vurugu zilizotokea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde zilizohusisha waumini wa kanisa hilo.

Hata hivyo kanisa hilo ambalo alikuwa anatumia kama makao makuu aliyekuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk Edward Mwaikali limefungwa na waumini wanaomuunga mkono Askofu mpya, Geofrey Mwakihaba

Ofisa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Johanes Bitegeko akiwa na askali wengine waliingia maeneo ya kanisa hilo na kuwatawanya waumini waliokuwa wamekusanyika makundi mawili tofauti wanaomuunga mkono Askofu Mwakihaba na Dk Mwaikali.

Akizungumza eneo la tukio, Bitegeko amesema mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na kuwataka watu wote kutawanyika akisema bado unashughulikiwa.

"Sina mambo mengi, kazi yetu ni kushughulikia usalama, mmekusanyika bila sababu za msingi tunaomba muondoke muendelee na shughuli za uzalishaji" amesema Ofisa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live