Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Amani ya Maaskofu na Maashekhe yamuonya Askofu Gwajima

98041 Gwajima2+pic Kamati ya Amani ya Maaskofu na Maashekhe yamuonya Askofu Gwajima

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamati ya Kitaifa ya pamoja kwa Maaskofu na Maashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Tanzania imemkemea Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kutoana madai ya kusambaza kipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma chenye lengo la kuhamasisha watu kuunda kikundi cha kikabila nchini. Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 05, 2020 na mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu William Mwamalanga imesema kuwa viongozi hao wa dini wanaungana na na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lililompa askofu huyo onyo kwa kuwa  ukabila ni dhambi hatari ambayo inapanda chuki ndani ya jamii na ni chukizo mbele za Mungu. Kamati hiyo imesema kuwa kitendo hicho kinapaswa kudharauliwa na kila Mtanzania na imelipongeza jeshi la polisi kwa kumpa onyo Askofu Gwajima. “Ndani ya jamii zetu mijini na vijijini kuna vikundi mbalimbali vya kimaendeleo vinavyoshirikisha makabila mbalimbali hutajawahi kuona polisi wanavikamata kwa kujiunga kwao bila shaka hili la Askofu Gwajima Polisi hawajakosea,” imesema sehemu ya taarifa hiyo. Gwajima alipewa onyo na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam baada ya jeshi hilo kujiridhisha na kosa la kusambaza kipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma zenye lengo la kuhamasisha watu kuunda kikundi cha kikabila nchini. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo limesema kabla ya Gwajima kupewa onyo walimhoji na baadaye kumuonya kuacha mara moja vitendo vya kuligawa Taifa kwa kutumia vigezo vya ukabila Kipeperushi hicho chenye picha ya Rais John Magufuli kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kikiwa na maandishi yanayosomeka kwa lugha ya kisukuma. Pamoja na kipeperushi hicho, inadaiwa Askofu Gwajima pia alitoa ujumbe wa sauti wenye ujumbe wa kumpongeza Rais Magufuli na kuhamasisha wasukuma kurejesha utamaduni wao wa zamani wa kutumia lugha yao, kusaidiana katika shida na raha.

Chanzo: mwananchi.co.tz